Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Mtandao wa Wezi wa Magari Wanaswa Pwani
Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linawashikilia Watu wawili Ally Selemani, Mkazi wa DSM na Geoffrey Lusekelo Mkazi wa Mbeya Kwa kosa la wizi wa gari aina ya Toyota Raum lenye namba za usajili T 256 DCV lililokamatwa maeneo ya Bwawani Kata ya Ubena Wilaya ya Kipolisi Chalinze Mkoani Pwani.

 

RPC Pwani, Wankyo Nyigesa amesema uchunguzi unaonesha hapo awali gari hilo lilitolewa Dar es salaam likiwa na namba za IT likisafirishwa kwenda Nchi jirani na Watuhumiwa hao walipofika maeneo ya Bwawani waliliwekea namba za usajili wa Toyota Rav 4 na huku chassis namba zikiwa zimefutwa, uchunguzi unaendelea na utakapokamilika Watuhumiwa watafikishwa Mahakamani.


 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments