Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Mwili wa Baba Yake Bashe Wawasili na Kuzikwa Usiku NzegaMWILI wa Marehemu Sheikh Mohamed Bashe umepumzishwa usiku wa kuamkia leo katika Makuburi ya Waislamu Kitongo Mjini Nzega Mkoani Tabora.
Akizungumza kwa niaba ya familia Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe ambaye ni mtoto wa marehemu amesema familia inashukuru mchango wa jamii ya wakazi wa Nzega kwa namna walivyojitokeza kushiriki na familia katika mazishi hadi maziko ya baba yake.
Kabla ya mazishi imefanyika ibada ya kuuaga mwili wa marehemu Sheikh Bashe iliyoswaliwa katika Msikiti wa Ijumaa mjini Nzega.
Viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali wakiwemo mawaziri wamefika nyumbani kwa Naibu Waziri Bashe mjini Nzega ambapo wamejumuika pamoja na waombolezaji wengine kuupokea mwili huo.


 Sheikh Mohamed Bashe alifariki Novemba 23, 2021 nchini Afrika Kusini alikokuwa akipatiwa matibabu.

 Download Our Udaku Special APP Kutoka Google Play Store Kwa Kutumia Link Hii Hapa>>>

Post a Comment

0 Comments