Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Nandy awa kivutio uzinduzi wa Guinness Smooth kanda ya Nyanda za juu kusiniMsanii wa muziki wa kizazi kipya Nandy ambaye pia ni balozi wa bia ya Guinness Smooth, alikuwa kivutio kikubwa kwa wanafunzi wa vyuo mkoani Mbeya ambao walihudhuria uzinduzi wa bia mpya aina ya Guinness Smooth.

Nandy alifanikiwa kuteka mioyo ya wanafunzi walijitikeza kwa wingi katika uzinduzi wa Guinness Smooth ambao walionekana kuwa na kiu kubwa ya brudani ambayo alifanikiwa kuikata

Akiongea katika tukio hilo la uzinduzi, meneja chapa wa SBL Ester Raphael alisema baada ya uzinduzi wa Guinness Smooth bia hiyo sasa itapatikana kwa wingi katika eneo lote la kanda ya Nyanda za juu kusini kwa shilingi 1,500 tu.

Msanii Nandy  akitumbuiza mbele ya umati wa watu wakati wa uzinduzi wa bia mpya ya Guinness Smooth mkoani Mbeya.


Meneja masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti Denis Tairo akimkabidhi zawadi mmoja wa wanafunzi aliyejitokeza katika uzinduzi wa bia mpya ya Guinness Smooth jijini Mbeya.
Baadhi ya washindi wa kuimba na kucheza wakiwa wamekabidhiwa zawadi zao katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kampuni ya bia ya Serengeti


Baadhi ya wanafunzi wa vyuo mbali mbali mkoani Mbeya wakiifurahia bia mpya ya Guinness Smooth mara baada ya kuzinduliwa rasmi mkoani humo na eneo zima la kanda ya Nyanda za juu kusini

 Download Our Udaku Special APP Kutoka Google Play Store Kwa Kutumia Link Hii Hapa>>>

Post a Comment

0 Comments