Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Polepole Atoa Mpya "Sina Mpango Kugombea Ubunge 2025"
Mbunge Humphrey Polepole ameweka wazi kwamba hana mpango wa kuwania nafasi ya ubunge wa jimbo ifikapo 2025 kama ambavyo baadhi ya watu wamekuwa wakimhoji kwa kile alichoeleza kuwa ni kazi ambayo hana utume nayo lakini ameomba watu walio na hofu ya Mungu kujitokeza kuwania nafasi hizo.

"Watu wengi wanasema we Bwana vipi ujue ni mbunge wa kuteuliwa ,vipi kuhusu jimbo? Sasa niwatangazie sina hata mpango wa kugombea jimbo kwa sababu si kitu ninahisi nina utume nacho kwa hiyo sitaki labda kuwa mbunge wa jimbo mahali fulani sitaki.

Ninaweza kuhudumu kwa namna nyingine huu ubunge wa kuteuliwa ikifika 2025 namshukuru Rais kwa kweli kama itafika huko au kama haitafika pia nitashukuru lakini naomba watu wengi zaidi muingie kwenye kugombea kwa sababu tukipata watu wengi wenye hofu ya Mungu hasa wanaotoka huku Kanisani tutakuwa na amani kuwa hamtarubuniwa na mtatenda haki"-Humphrey Polepole.

 Download Our Udaku Special APP Kutoka Google Play Store Kwa Kutumia Link Hii Hapa>>>

Post a Comment

0 Comments