Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Polisi Yanasa Genge la Wahalifu DarJeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawasikilia watuhumiwa nane kwa tuhuma za kijihusisha na vitendo vya kihalifu vinavyohusisha unyang’anyi wa kutumia nguvu, silaha na kuvunja nyumba usiku pamoja na kuwafunga kamba na walinzi kisha kuiba.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema katika oparesheni maalum jeshi hilo pia limefanikiwa kuzima jaribio la wizi wa gari aina ya IST lenye namba za usajili T 374 DKR katika eneo la Kimara ambapo katika kukabiliana na wahalifu hao waliojaribu kuwarushia risasi askari, jambazi mmoja amejeruhiwa na baadaye kupoteza maisha.

Kamanda Muliro amesema wizi wa magari madogo hasa aina ya IST bado unaendelea na kwamba jeshi la polisi halitakuwa na huruma na mtu yoyote atakayejaribu kutishia askari wakati wanatekeleza majukumu yao.

 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments