Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Rais wa Shirikisho la Soka Kenya Nick Mwendwa Akamatwa
Rais wa Shirikisho la Soka la Kenya Nick Mwendwa amekamatwa, vyombo vya habari nchini humo vinaripoti.


Ripoti za kukamatwa kwake zimechapishwa na runinga za NTV na Citizen kupitia mitandao ya kijamii .Inasemekana Mwendwa alichukuliwa na maafisa wa polisi waliovalia nguo za kiraia siku moja baada ya waziri wa Michezo Amina Mohamed kuvunja shirikisho hilo na kuunda kamati ya muda ya wanachama 15.Jaji mstaafu Aaron Ringera aliteuliwa kuwa mwenyekiti wa kamati hiyo ambayo majukumu yake katika kipindi cha miezi sita ni pamoja na kuendesha masuala yote ya FKF.Hatua hiyo inafuatia mapendekezo ya kamati ya ukaguzi aliyounda kuchunguza shirikisho la soka nchini humo linalokabiliwa na tuhuma za ufisadi na utawala mbaya .Jaji mstaafu Aaron Ringera anasema kamati ya muda ya FKF imeamua kwa kauli moja kusimamisha Ligi Kuu ya FKF, Ligi Kuu ya Kitaifa, Ligi ya Daraja la 1, Ligi Kuu ya Wanawake na Ligi ya Daraja la 1 ya Wanawake kwa muda wa wiki mbili.


 Download Our Udaku Special APP Kutoka Google Play Store Kwa Kutumia Link Hii Hapa>>>

Post a Comment

0 Comments