Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Rapa Travis Scott Kugharamia Mazishi ya Waliofariki na Kurudisha Hela za Mashabiki


Rapa Travis Scott anaendelea kuwajibika kufuatia janga lililotokea kwenye tamasha lake ambalo lililofanyika November 5 mwaka huu ambapo watu 8 walifariki dunia na wengine wengi kujeruhiwa. Kwa mujibu wa tovuti ya TMZ, Travis Scott atagharamia gharama za mazishi ya watu wote 8 waliofariki. Aidha ameahidi kuwapa msaada wa Kisaikolojia waathirika wote akishirikiana na kampuni ya BetterHelp.

Mbali na hilo, tovuti ya Variety imeripoti kwamba Travis Scott pia atarudisha pesa kwa wahudhuriaji wote wa tamasha hilo - Astroworld Music Festival. Juzi shabiki mmoja alijitokeza na kumfungulia mashtaka rapa huyo pamoja na kampuni ya Live Nation na Drake, akidai fidia ya ($1 million) zaidi ya TSh. Bilioni 2.

 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments