Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Ray C Atema Nyongo: Vita ya Harmo na Mondi Itasababisha Mauti

Kwa haraka haraka tu kama hichwa chako kunafanya kazi! Unadhani mwisho wa haya yanayoendelea utakuwa ni nini? Kwangu naona mauti tu mbeleni… neno baya sana hili na linaogopesha ila huu ndio ukweli.

 

Kwenye muziki beef za hapa na pale zipo ila hii ni zaidi ya beef, hii ni vita moja kubwa ya kushushana na kuharibiana brands… na nasema hili kwa pande zote mbil. Sio kitu cha sisi Watanzania kukifurahia hata kidoco kama kweli tunawakubali kwa moyo mmoja hawa wasanii wawili.

 

Hawa ndio wanaopeperusha bendera kwa sasa bila ubishi… Sasa mkiendelea kusapoti hii bifu mwisho wake utakuwa mbaya…

 

Hisia zangu sio nzuri kuhusu yanayoendelea… nadhani kuna wakubwa wakuweza kuwatuliza hawa. Nadhani watu wakubwa serikalini nao wako shocked… Ni muda mzuri wakuwaita hawa wawili na kuongea nao… this is not good at all, na uhakika linawezekana. Wakubwa Serikalini natumaini mtaiona MSG hii, ni zaidi ya vita.

 

Ninauhakika wengi wanafurahia wapate cha kuongea ila kama kweli, mnathamini wasanii wa Tanzania na mnafurahi wanavyoiwakilisha Tanzania kama msifiavyo mara kwa mara basi nina uhakika wakubwa mtasuluhisha hili tatizo kati ya hawa wasanii wawili. I have a bad feeling about this… Do something.

 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments