Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Rio Ferdinand Amkataa Kocha Ole Gunnar Solskjaer wa Manchester United, Atimuliwe tu Hana Jambo


Mustakabali wa kocha Ole Gunnar Solskjaer ndani ya Manchester United umetiliwa shaka na beki wa zamani wa klabu hiyo na timu ya taifa ya Uingereza, Rio Ferdinand ambaye sasa amemtaka “ampishe mkufunzi mwingine”.

Solskjaer amekuwa katika presha kubwa ya kutimuliwa ndani ya Old Trafford tangu kikosi chake kipasuke 5-0 na Liverpool kisha 2-0 na Manchester City katika Ligi Kuu Uingereza (EPL).

Akizungumza katika kipindi chake cha YouTube cha ‘Vibe with Five’, Ferdinand alisema huu ndio wakati mwafaka zaidi kwa Solskjaer kubanduka Man United kwa kuwa “ataondoka akiwa na hadhi pamoja na kitu cha kujivunia”.

Ferdinand, 43, ambaye alichezea Man United kwa kipindi cha miaka 12 na kukizolea kikosi hicho mataji sita ya EPL, ameendelea kusema; “Kuanzia alikotutoa kama kikosi hadi tulipokuwa mwanzoni mwa msimu huu, nadhani Solskjaer alifanya kazi ya kuridhisha mno,” akatanguliza.

“Lakini mahali tulipo kwa sasa si pazuri. Itakuwa vema akiondoka kwa heshima badala ya kusubiri kutimuliwa wakati ambapo mazuri yote ambayo amefanyia klabu yatakuwa yameyeyushwa na msururu wa matokeo duni,” akaongeza Ferdinand.


Man United kwasasa wanashika nafasi ya sita kwenye msimamo wa jedwali la EPL kwa alama 17, tisa nyuma ya Chelsea wanao seleleka kileleni.

 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments