Ticker

6/recent/ticker-posts


 

Samatta azaliwa upya, Antwerp yamuangusha EUROPA

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE


Mshambuliaji na Nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta ameifungia timu yake ya Royal Antwerp bao dakika 88’ na kulazimisha sare ya 2-2 dhidi ya Eintranch Frankfurt usiku wa jana kwenye michuano ya Ligi ya Europa.

Sare hiyo imeifanya Royal Antwerp iwe na alama 2 tu kwenye michezo yake 5 na kushika mkia wa kundi D nyuma ya Fenerbahce yenye alama 5, ya pili Olympiacos yenye alama 9 na Frankfurt akiwa kinara na alama 11.

Bao hilo la Samatta kufunga mabao 3 kwenye michezo 5 aliyoicheza kwenye michuano hiyo na kuanza kurejesha kiwango chake cha ufungaji lakini timu yake haijafanikiwa kusonga mbele hatua ya mtoano inayofuata ya 32 bora ya Europa.

Kinara wa kundi hilo, Frankfurt amefuzu hatua inayofuata ya mtoano ya 32 bora wakati Royal Antwerp na Fenerbahce zikiwania kumaliza kwenye nafasi ya tatu ili zicheze Uefa Europa Conference Ligi ili zisiambulie patupu.

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments