Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Samia: Mgao wa Maji Umetokana na Ubishi“Natambua Miji yetu mingi mikubwa ina uhaba wa maji unaopelekea uhaba wa maji na upungufu wa umeme hali hii inatokana na ubishi na ukaidi wa Wanadamu na kudra za Mwenyezi Mungu”

“Ubishi na ukaidi ni kuwa bado Wananachi wengi wameendelea kuvamia vyanzo vya maji kwa kuchepusha maji kwa ajili ya kilimo na kulima karibu na vyanzo vya maji haya yote yanafanya mtiririko wa maji kupungua, mfano Dar es salaam wanatumia Ruvu Juu na Ruvu Chini, kima cha maji Ruvu chini kimepungua kwa nusu na mchakato wa kupeleka kwa Wananchi umepungua ndio maana Dar es salaam kumekuwa na mgao wa maji”

“Tulipoenda kutazama tumekuta Watu wanachepusha maji kwa ajili ya kilomo n.k na kingine ni uhujumu wa makusudi kuzuia maji kwenda kwa Wananchi maana yamewekwa hadi magogo, baada ya kuendesha oparesheni jana na leo wanaendelea pamoja na kutoa mchanga tunategemea Dar es salaam watapata maji, kutakuwa na mgao wa maji lakini utapungua”

Maneno ya Rais Samia Suluhu leo kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya Hospitali ya Bugando Mwanza.

 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments