Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Siku ya Leo Kwa Mara ya Kwanza Mwanamke Anaenda Kuwa Rais wa Marekani Kwa Muda..Sababu Hizi Hapa


Siku ya leo Novemba 19, 2021 itaingia kwenye vitabu vya kumbukumbu kwani kwa mara ya kwanza Mwanamke atakuwa na nguvu au mamlaka ya Urais (presidential power) katika historia ya taifa la Marekani. Mwanamama Kamala Harris ambaye ni makamu wa Rais, leo Ijumaa atakabidhiwa kwa muda madaraka ya Urais ambapo imetajwa kuwa atahudumu kwa takribani dakika 30 hadi 40.

Hii imekuja kufuatia Rais Joe Biden kuwasili katika kituo cha matibabu cha Walter Reed ambapo ameenda kufanyiwa vipimo vya mwili (body check-up) zoezi ambalo hulifanya kila mwaka kutokana na umri wake hivyo atachomwa sindano ya ganzi wakati akifanyiwa kipimo cha utumbo mpana. Kwa mujibu wa wataalamu, inaelezwa kuwa binadamu akichomwa ganzi hiyo, hupoteza uwezo wa kiakili kwa asilimia 100.

 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments