Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

St Anne Marie kumsomesha aliyeongoza kitaifa darasa la saba

Mwanafunzi bora kitaifa kwenye matokeo ya darasa la saba mwaka huu, Eluleki Haule akionyesha cheti alichokabidhiwa na shule yake ya St. Anne Marie kumshukuru kwa  kushika nafasi hiyo kwenye hafla ya kumpongeza iliyofanyika mwishoni mwa wiki Mbezi Kimara kwa Msuguri Dar es Salaam.

Mwanafunzi bora kitaifa kwenye matokeo ya darasa la saba mwaka huu, Eluleki Haule akimlisha keki Mkurugenzi wa shule za St. Anne Marie Acdemy, Dkt. Jasson Rweikiza wakati wa sherehe ya kumpongeza kwa kushika nafasi hiyo iliyofanyika shuleni hapo mwishoni mwa wiki. Dkt. Rweikiza ameahidi kumsomesha hadi kidato cha sita.

 Mwanafunzi bora kitaifa kwenye matokeo ya darasa la saba mwaka huu, Eluleki Haule akkata keki katuka sherehe iliyoandaliwa na St Anne Marie kumpongeza kwa kufanikiwa kuwa wa kwamza kitaifa kwenye matokeo ya darasa la saba mwaka huu.

Na Mwandishi Wetu
MWANAFUNZI aliyeongoza kitaifa kwenye matokeo ya darasa la saba ameula baada ya shule aliyosoma ya St Anne Marie Academy kuahidi kumsomesha bure hadi kidato cha sita.

Ahadi hiyo imetangazwa mwishoni mwa wiki na Mkurugenzi wa shule hiyo, Dk. Jasson Rweikiza wakati wa hafla iliyoandaliwa na shule hiyo kumpongeza kutokana na ushindi wake.

Hafla hiyo imehudhuriwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kagera na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam, Kheri James.

Dk. Rweikiza amesema mbali na kumsomesha bure shule hiyo itampa shilingi 3,000,000, kumpeleka kumtambulisha bungeni Dodoma yeye na wazazi wake na kubandika picha yake kwenye magari yote 51 ya shule hiyo.

Amewataka wanafunzi wahitimu kuacha kubweteka huku akiwasisitiza kusoma na kujituma kwa bidii ili waweze kufanya vizuri katika kasomo yao na mitihani kwa ujumla.

“Niwashukuru walimu kwani walipambana sana hadi kufanikiwa kupata mafaninikio haya, pia nimshukuru Mkuu wa shule kwa uongozi boro pamoja na wanafunzi wote waliofanikiwa kufanya vizuri katika mitihani yao na niwasisitize muendelee kusoma kwa bidii kwani taifa linawategemea,” alisema Rwaikize.

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, KheriJames alimpongeza Eluleki Haule na kumtaka aendelee kufanya vizuri kwenye masomo yake ya sekondari.

Amesema kwa matokeo hayo ni ishara kwamba wazazi na walimu wanatimiza majukumu yao huku akitoa wito kwa wazazi walezi na jamii kuwalea watoto katika maadili mema na kutoa kipaumbele kwenye elimu ili badae wajisaidie na kulisaifia taifa kwa ujumla.

“Kwa niaba ya serikali tunampongeza Kijana Haule kwa kuwa Tanzania one kwa mwaka huu. Leo Tanzania nzima wanaijadili St. Anne Marie kwasababu ya mtoto huyu, hii ni safari ya kwanza ambayo umeanza tunatarajia utafanya vizuri zaidi katika ngazi zinazoendelea.” alisema James.

 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments