Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

TANZIA: Aliyekuwa Mkufunzi DSJ afariki
TANZIA: Aliyekuwa Mkufunzi DSJ afariki
UONGOZI wa Chuo cha Uandishi wa Habari Dar es Salaam (DSJ), umetangaza kifo cha aliyekuwa mkufunzi wa mtaalamwa kozi ya ‘Public Relations and Advertising’ na ‘Entrepreneurship’ chuoni hapo, Joyce Mbogo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kifo cha Joyce kimetokea leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, jijini Dar es Salaam.

Marehemu Joyce atakumbukwa katika tasnia ya habari hususan Uhusiano kwa umma, utangazaji, na matangazo.

Watu mbalimbali waliofanya kazi na marehemu Joyce, na aliowafundisha, wameeleza kupokea taarifa za msiba huo kwa masikitiko makubwa, huku wakiukumbuka urafiki, ucheshi, ukarimu, usikivu na ushirikiano aliowaonyesha na kwa watu wengine nje ya kazi.

 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments