Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Tisa wajeruhiwa ajali ya gari Handeni
Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga limesema watu tisa wamejeruhiwa katika ajali ya gari aina ya Prado iliyotokea katika eneo la Michungani wilayani Handeni baada ya gari hilo kupinduka.


Akizungumza na Mwananchi Digital Jumamosi Novemba 13, 2021, Kamanda wa Polisi mkoa huo, Safia Jongo amesema ajali hiyo imetokea leo saa mbili asubuhi baada ya gari hilo lililobeba watu tisa kugonga kingo ya barabara na kupinduka."Dereva wa Prado amegonga ukuta wa barabarani na gari kupinduka na kusababisha abiria wote tisa kujeruhiwa, wamekimbizwa hospitali kwa matibabu zaidi "'amesema Kamanda Safia Jongo.


 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments