Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Ushahidi wa Inspekta Maulid kesi ya kina Mbowe huu hapa
Shahidi wa nne wa upande wa mashtaka katika kesi ndogo ndani ya kesi ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu leo ametoa ushahidi katika Mahakama Kuu ya Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.


Kesi hiyo ndogo inatokana na mshtakiwa wa tatu Mohamed Ling’wenya kupinga maelezo ya onyo yaliyotolewa na shahidi wa nane katika kesi ya msingi, SP Jumanne, akidai hakuwahi kufikishwa Kituo Kikuu cha Polisi, Dar es Salaam ila alilazimishwa kusaini maelezo ambayo hakuyatoa.Inspekta Issa Maulid anaapa kwaajili ya kuanza kutoa ushahidiAnaongozwa na wakili wa Serikali Robert KidandoWakili Kidando: Unafanya kazi ganiShahidi: Ni askari polisiADVERTISEMENTWakili: Unazifanyia wapi?Shahidi: Nazifanyia Kikosi cha Polisi Tazara Dar es Salaam.Wakili: Umesema uko Kikosi cha Reli Tazara, kikosi chako cha kazi ni kipi?Shahidi: Pugu road na sasa ni Kaimu mkuu wa kituo cha PuguShahidi: Majukumu haya nilikabidhiwa toka tarehe 3/6/2021 na majukumu yangu ni kusimamia askari ninaowaongoza na kusimamia majuku yangu ikiwemo kusimamia askari kutimiza majukumu waliyopewaShahidi: Jukumu lingine ni kusimamia doria, mali za Serikali yakiwemo majengo magari samani na silaha na mali zingine zote.Shahdi: Jukumu la nne ni kushughulikia malalamiko yote yanayofikishwa kituoni ikiwemo kufungua kesi kupeleleza na kuwafikisha mahakamani watuhumiwa, kusimamia mahabusu walioko kituoni kujua hali zao za kiafya, kuhakikisha wamepata huduma za chakula kwa wakati.Shahidi: Kila inapofika asubuhi nakagua mahabusu na kukagua kitabu cha kumbukumbu za mahabusu (DR) nikiwa nimeongozana na askari wawili mmoja wa kike na mwingine wa kiume.Shahidi: Baada ya kufika mahabusu naanza kuita jina moja baada ya lingine. Baada ya kumuita namuhoji kosa tarehe aliyoingia nalinganisha na yaliyoandikwa kwenye kitabu.Shahidi: Dhumuni la kuwahoji ni Ili kufahamu kilichaoandikwa kwenye kitabu na kujiridhisha kisha narudi kwenye chumba cha mashtaka na kusaini kitabu.Shahidi: Malengo ya kufanya ukaguzi ni kuainisha taarifa na idadi ya mahabusu, pia kufanya upelelezi na kukamilisha endapo upelelezi utakuwa umekamilika naamuru washtakiwa wapelekwe mahakamani.Shahidi: Kama ukaguzi bado ukamilishwe kwa wakati na endapo mtuhumiwa ana haki ya kupewa dhama adhaminiweShahidi: Tazara najihusisha na makosa yote ya jinai yanayotokea, Maeneo yote (within compound) katika station zake, karakana zake na ofisi zake.Shahidi: Mpaka sasa nina miaka 17 TazaraWakili wa Serikali: Ongeza sautiShahidi: Kuanzi Mei 10, 2020 nilikuwa operation officer wa Kikosi cha Tazara kuanzia Dar es Salaam hadi TundumaShahidi: Majukumu yangu makubwa yalikuwa ni kupata taarifa za mahabusu walioko kwenye vituo vyote na kutoa taarifa, kusimamia mazoezi ya utayari kwa askari wote ,Shahidi: Agost 2,2020 nlipewa barua ya kukaimu Mkuu wa kituo cha Tazara baada ya aliyekuwepo kwenda likizo ya siku 20Shahidi: Kuanzia Agosti 3 hadi Septemba 6, 2020 nilikaimu nafasi hiyo ambapo mkuu wa Kituo Richard Obutu aliiacha.Shahidi: Majukumu niliyokuwa nayo ni kusimamia nidhamu.Shahidi: Katika Majukumu yangu kuna kitabu cha kufungulia taarifa, kitabu cha kuandika kumbukumbu za mahabusu (DR) na kitabu cha kunakili mali anazokutwa nazo mtuhumiwa baada ya kufanya upekuzi.Shahidi: Nakumbuka Agost 7,2020 nilifanya ukaguzi kama inavyopaswa katika mahabusu hapakuwa na mtuhumiwa hata mmojaShahidi: Agosti 8,2020 nilifanya ukaguzi alikuwepo mtuhumiwa mmoja mwanaume aliyekuwa mtumishi wa SerikaliShahidi: Agosti 9,2020 palikuwa na watuhumiwa wawili, wanafunzi wa kiume ambao walikuwa wanatuhumiwa kuhatarisha miundo mbinu ya Reli, tuliwakamata wakifungua nati za Reli.Wakili wa Serikali: Ulibaini vipi hao watuhumiwa?Shahidi: Kama ilivyo kawaida inapofika asubuhi napitia Detention Register na katika ukaguzi nilijiridhisha mahabusu hao wapo.Wakili wa Serikali: Sasa Baada ya Kufanya Shughuli hiyo ya Ukaguzi wa Mahabusu, wewe unauthibitisho gani kama watuhumiwa hao walikuwepoShahidi: Udhibitisho wangu mkubwa katika ukaguzi ni kitabu cha kumbukumbu za mahabusu (DR). Kipindi ambacho na Kaimu kitabu hicho kilikuwa kinatunzwa charge roomShahidi: Niliendelea kukaimu hadi Septemba 6,2020 aliporudi Richard ObutuShahidi: Nimkabidhi mali kama nilivyoorodhesha silaha,magari, samani, mahabusu waliokuwepo na nyaraka za siri za Serikali. Vitabu vilivyokuwa vinatumika ikiwemo DR havikuingia kwenye makabidhiano vilibaki CROWakili Kidando: Ulikaimu tena nafasi hiyo kutoka kwa nani?Shahidi: Kwa Richard Obutu ambaye amehamishiwa Zanzibar.Wakili: Kwanini ulikabidhiwa majukumu hayo?Shahidi: Baada ya SP Richard Obutu kuhamishwa.Wakili: Makabidhiano hayo yalifanyikaje?Shahidi: Kwa nyarakaWakili: Ulikabidhiwa nini?Shahidi: Magari, silaha nyaraka za siri, na  vitabu vingine mbalimbali ikiwemo DRWakili: DR ulizokabidhiwa zipi?Shahidi: Miongoni mwa DR nilizokabidhi ni pamoja na zilizotumika ambazo nimezihifadhi.Shahidi: Novemba 14 alikuja mtu kutoka ofisi ya DI aliyejitambulisha Inspekta Swilla, nikiwa ofisini kwangu, nikaambiwa naitwa chini.Shahidi: Baada ya kuonana nae alinihoji kuhusu DR iliyotumika Agosti 7,8,9 , 2020 na kunieleza kuwa inahitajika mahakamani kwa ajili ya kutolea ushahidi. DR hiyo ilikuwa imetumika na kuisha tangu Machi 2021 kwa hiyo hazikuwepo CRO.Shahidi: Baada ya kuondoka nilirudi na kuitafuta nilipoikagua nikakuta Agost 7,2020 hapakuwa na mahabusu, Agosti 8,2020 palikuwa na mmoja na Agosti 9 palikuwa na wawili.Wakili wa Serikali: Kuna kesi ipo hapa Mahakamani hebu niambie kama kuna majina ya Halfan Bwire Hassan na Adam Kasekwa.Shahidi: Kupitia DR ya tarehe hizo washtakiwa waliopo mahakamani hawakuwepo.Wakili: Mheshimiwa Jaji tunaomba kumkabidhi Shahidi kielelezo kwaajili ya utambuzi?Wakili: Hiyo ni nini?Shahidi: DR ya Pugu roadWakili: Umeitambuaje?Shahidi: Kwa maandishi yaliyoko njeWakili: Utakitambuaje?Shahidi: WEF01 Januari 1/2019. Ndani kuna kumbukumbu namba zilizoandikwa kwa kifupiWakili: Unataka Mahakama ifanye nini?Shahidi: Ipokee kama kielelezoBaada ya mawakili wa utetezi kupitia kitabu cha kumbukumbu ya mahabusu (DR ) Wakili wa mshtakiwa wa kwanza, wa pili, wa tatu na wanne hawana pingamizi.Jaji: Napokea  kama kielelezo p3 kwenye Kesi ndogo ndani ya kesi kubwa ya upande wa mashitakaKielelezo kimepokewa na mahakama kielelezo namba tatu cha upande wa mashtaka katika kesi ndogo.Wakili wa Serikali: Kitabu hicho kilitumika kuanzia lini hadi liniShahidi: Kuanzia 01.01.2019 Mpaka 29 May 2021Wakili wa Serikali Kidando amemaliza.


 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments