Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Utata Bilionea Aliyemhonga Mpenzi Wake Sh2.3 Bilioni
Merc De Mesel ambaye anatajwa kuwa miongoni mwa mabilionea, amelalamikia kitendo cha mpenzi wake kusumbuliwa baada ya kumwekea kiasi cha Sh2.3 bilioni kwenye akaunti yake ya benki.


Pia, amelalamika kwa namna alivyohusishwa kuwa anajihusisha na shughuli zisizo halali huku mamlaka za Kenya zikizuia kwa siku kadhaa akaunti ya mpenzi wake mwenye umri wa miaka 21 raia wan chi hiyo.Ripoti zilizoripotiwa na vyombo vya habari vya Kenya zinasema kuwa Mesel amejikusanyia utajiri mkubwa na amekuwa bilionea wa bitcoin, ambaye alianza kufanya biashara kwa sarafu za mtandao mwaka 2008.Katika video iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii inamuonyesha bilionea huyo akieleza kuwa amemzawadia mpenzi wake mabilioni hayo kwa kufuata taratibu zinazotakiwa ikiwa ni pamoja na kujaza nyaraka za benki.Mara ya kwanza Msel alimuwekea mpenzi wake huyo Agosti 4, 2021 kwa kuweka kiasi cha Ksh25,803,756 kisha Agosti 5 akaweka Ksh25,803,756 na mara ya tatu na ya nne iliingiza KSh25,242,756 na Ksh25,579,356 ikiwa ni Agosti 6, mwaka huu.Baada ya kiasi hicho cha feda kuingia katika akaunti ya binti huyo, wapelelezi kutoka Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai walivamia nyumba kwao na kuwakamata, wakimtuhumu kujihusisha na shughuli zisizo halali, lakini Mesel aliwatoa kofu na kuwataka kutulia akisisitiza kuwa amekuwa na mpenzi huyo kwa muda mrefu.Mesel aliongeza kuwa wakati watu wa kutoka idara ya upelelezi walipovamia nyumbani kwao mpenzi wake huyo alikuwa na ujazito mkubwa.“Nilijua kuna shughuli nyingi zisizo halali barani Afrika kuliko Ulaya, lakini nilivamiwa nyumbani kwangu ghafla bila taarifa wala kuitwa polisi au kuulizwa maswali. Nilikamatwa wakachukua simu na hati ya kusafiria, wakanichukua na pingu mimi pamoja na mpenzi wangu ambaye ni mjamzito. Sikutarajia kitu kama hicho kutokea” amesema na kuongeza kuwa kitendo hicho kimemfanya ahisi yeye na mpenzi wake hawako sehemu salama kuishi.

 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments