Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Wanawake wa Aina Hii Wana Ukimwi


WANAWAKE sita kati ya Kumi wanaotumia dawa za kulevya wameambukizwa Virusi Vya Ukimwi kutokana na kuchangia sindano za kujidunga, kwa mujibu wa utafiti uliofanyika mwaka 2014 ukihusisha wanawake 100.

Hayo yameelezwa na Kamishna wa Kinga na Tiba wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA), Dk Peter Mfisi, katika kikao kazi cha waandishi wa habari za Kidigitali kilichoandaliwa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) mkoani Morogoro.

Dk Mfisi amesema changamoto ya unyanyapaa ndio chanzo kikuu cha warahibu wanawake nchini walioathiriwa na VVU kushindwa kufika katika vituo vya matibabu.

 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments