Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Wanawake wawili wamshtumu baba yake Waziri Mkuu wa Uingereza kuwagusa vibaya bila ridhaa yao
Wanawake wawili akiwemo mbunge wa chama cha Conservative wamemshutumu baba yake waziri mkuu wa Uingereza, Stanley Johnson kwa kuwagusa isivyostahili.


Caroline Nokes ameiambia Sky News kuwa bwana Johnson alimshika kwa nyuma kwa nguvu wakati wa mkutano wa chama cha Tory mwaka 2003.Na mwandishi wa siasa Ailbhe Rea anamshutumu bwana Johnson kwa kumpapasa bila ridhaa yake katika mkutano wa chama cha Conservative mwaka 2019.Bwana Johnson ameiambia Sky kuwa hakumbuki kufanya jambo kama hilo kwa bi. Nokes.Bi Nokes, Mbunge wa Romsey na Southampton North tangu mwaka 2010, alikuwa mgombea wa chama cha Conservative wakati tukio hilo lilipotokea katika mkutano wa mwaka 2003 huko Blackpool.


 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments