Ticker

6/recent/ticker-posts

Wasanii Hawa Wajitafakari Sana Kuhusu Mashairi yaoKatibu mkuu wa wizara ya sanaa,utamaduni na michezo, Dr. Hassan Abas amejibu swali la mtangazaji wa Clouds Fm, @kenedytheremedy alilouliza kama mheshimiwa kwenye Playlist yake ana nyimbo za @roma_zimbabwe na @naytrueboytz na kama anazo ni zipi.

Dr. Abas amedai hana kumbukumbu ni nyimbo ngapi anazo au anazipenda kutoka kwa wasanii hao ila amedai anapenda wimbo mmoja wa Roma unaitwa Zimbabwe. Pia Dr. Abas amedai wasanii hao wajitafakari mashairi wanayoandika kama wanataka kuwa walalamishi tu (wanaharakati) ama wanamuziki wanaotaka kwenda mbele na kuendeleza sanaa zao.

Kingine Dr. Abas amedai ikiwa msanii atakuwa na nyimbo zenye maudhui mabovu na yenye kuikashifu serikali basi wasahau kuitwa kwenye matamasha ya serikali pia. Ameyazungumza haya akiwa Bagamoyo kwenye tamasha la kimataifa la sanaa na utamaduni.


Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments