Ticker

6/recent/ticker-posts


 

Watu 17 wajeruhiwa katika shambulizi la kisu ndani ya kituo cha treni Tokyo

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

Shambulio la kisu na moto kwenye njia ya treni ya chini ya ardhi mjini Tokyo limesababisha watu 17 kujeruhiwa, vyombo vya habari nchini humo vinasema.
Polisi walimkamata mwanamume mwenye umri wa miaka 24, ambaye alikuwa amevalia mavazi sawa na mhusika wa Joker kutoka kwa filamu za Batman.

Shambulio hilo lilitokea wakati watu wengi walipokuwa wakielekea kwenye sherehe za Halloween.

Shambulio hilo lilitokea mwendo wa saa 20:00 kwa saa za huko (11:00 GMT) karibu na kituo cha Kokuryo, katika vitongoji vya magharibi mwa mji huo. Walioshuhudia walisema mshukiwa alikuwa amevalia suti ya rangi ya zambarau na kijani.

“Nilifikiri ilikuwa ni mchezo wa Halloween,” shahidi mmoja aliambia gazeti la Yomiuri kuhusu shambulio hilo. "Kisha, nilimwona mtu akitembea huku, akipunga kisu kirefu polepole."

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments