Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Waziri wa Maji Jumaa Aweso Atinga Kwenye Ofisi za DAWASA Usiku wa Kuamkia leo


ziri wa Maji Jumaa Aweso usiku wa kuamkia leo ametinga kwenye Ofisi za DAWASA kuwekea msisitizo mambo mbalimbali kwenye kipindi hiki ambacho Dar es salaam imekumbwa na mgao wa maji ambapo mojawapo ya aliyoyasisitiza ni mgao wa maji kutolewa kwa uwiano na bila upendeleo.

Kwenye kikao hicho kirefu cha mikakati kilichofanyika usiku, Waziri @Jumaa_Aweso aliongoza majadiliano ya suluhu ya muda mfupi na muda mrefu ya tatizo hili la maji pamoja na kuwapa hamasa Watumishi katika kipindi hiki kigumu na kuwataka Wataalamu watumie ubunifu na maarifa yao yote usiku na mchana kuwasaidia Wakazi wa Dar es salaam.

Jambo jingine muhimu alilolisisitiza Waziri Aweso ni kuitaka DAWASA kutoa bei elekezi kwa watoa huduma binafsi wa maji kupitia magari (bowsers) na kumalizia kwa ahadi ya ushirikiano wa Wizara katika kukabiliana na changamoto zilizopo kwa DAWASA na Bonde la Wami Ruvu.

 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments