Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Yanga yaweka wazi hatma ya Ditram Nchimbi
Mkuu wa Idara ya Habari na  Mawasiliano wa klabu ya Yanga, Hassan Bumbuli amefunguka na kuthibitisha kuwa, Mshambuliaji Ditram Nchimbi bado ni mali ya Yanga kwani amesaliwa na mkataba wa mwezi mmoja.


Bumbuli amesema, "Ditram Nchimbi bado ni mchezaji wa Yanga bado anamkataba kwa leo wa tarehe 15 bado ana mwezi mmoja. Mpaka sasa hivi tunamhesabu kama mchezaji wetu na hayupo kambini kwasababu ana ruhusu maalum”.“Mkataba wake ukiisha kama tunamhitaji tunambakisha na kama hatutomhitaji basi tutamuaga kiungwana" Amesema Bumbuli”.Ditram Nchimbi alijiunga na Yanga misimu miwili iliyopita, lakini kuanzia mzunguko wa pili wa Ligi Kuu wa msimu 2020-21 alipoteza namba kwenye kikosi cha kwanza hivyo kuwa nje ya kikosi cha kwanza kwa muda mrefu.Jambo lililopelekea hata kuwa na takwimu mbovu za kutimiza mwaka mmoja bila kufunga bao lolote kwa klabu yake jambo ambalo pia linaelezwa litamfanya aoneshwe mlango wa kutokea hivi karibuni klabuni hapo.


 Download Our Udaku Special APP Kutoka Google Play Store Kwa Kutumia Link Hii Hapa>>>

Post a Comment

0 Comments