Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Young Africans Yasafiri kwa Basi Kuelekea Lindi
Kikosi cha vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara Klabu ya Young Africans msimu huu 2021/22, kwa mara ya kwanza kimesafiri kwa basi kutoka jijini Dar es salaam kuelekea mikoani.

Young Africans imeondoka Jijini Dar es salaam kwa usafiri wa basi kuelekea mkoani Lindi, ambako itacheza dhidi ya Namungo FC Jumamosi (Novemba 20), Uwanja wa Ilulu.

Young Africans ambayo itacheza nje wa Dar es salaam kwa mara ya tatu msimu huu 2021/22, imetumia usafiri huo kwa mara ya kwanza.

Michezo miwili dhidi ya Kagera Sugar na KMC FC ambayo ilichezwa mikoni, Kikosi cha Young Africans kilitumia usafiri wa ndege kwenda Kagera na Ruvuma-Songea.

 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments