Ticker

6/recent/ticker-posts


 

23 Waitwa Taifa Stars Kuivaa Uganda

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE
KOCHA Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars, Kim Poulsen, ametaja majina ya wachezaji 23 watakaoingia kambini leo Jumatatu kujiandaa na mchezo wa kirafiki wa kimataifa kusheherekea miaka 60 ya Uhuru dhidi ya Uganda.

 

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Desemba 9, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

Wachezaji hao ni Metacha Mnata (Polisi Tanzania), Haroun Mandanda (Mbeya City), Musa Mbisa (Coastal Union), Nathaniel Chilambo (Ruvu Shooting), Kelvin Kijiri (KMC), Hans Masoud (Coastal Union), Nickson Kibabage (KMC) na Oscar Masai (Geita Gold).

 

Wengine ni Abdulrazack Mohamed (KMC), Lusajo Mwaikenda (Azam), Abdulmajid Mangalo (Biashara United), Nashon Naftari (Geita Gold), Tariq Simba (Polisi Tanzania), Sospeter Bajana (Azam), Hassan Nassor (Dodoma Jiji) na Abdul Hamis Suleiman (Coastal Union.

 

Pia wapo Meshack Abraham (Kagera Sugar), Cleophace Mkandala (Dodoma Jiji), Denis Nkane (Biashara United), Rashid Juma (Ruvu Shooting), Vitalis Mayanga (Polisi Tanzania), Anuary Jabir (Dodoma Jiji) na Reliants Lusajo (Namungo).

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments