Ticker

6/recent/ticker-posts

Alikamwe "Mambo 10 nilioyaona Prison vs Yanga"1: USHINDI MUHIMU katika siku muhimu! Si rahisi kubeba pointi 3 dhidi ya Prison kwao.. Yanga wamezibeba huku baadhi ya wachezaji wakiwa na changamoto ya Afya! ✊ Mashabiki wa Yanga wana kila sababu ya kujivunia wapiganaji wao

2: Prison ni kama walikosa maandalizi mazuri ya saikolojia kuelekea kwenye mchezo huu. Presha ilikuwa Juu.. makosa binafsi ya wachezaji yakawa mengi katika maeneo muhimu

3: Nabi alibaki na system yake Lakini kulikuwa na 'Rotation' kwenye kikosi. Perfomance ya Makambo kwenye 'combination play' kwenye eneo la mwisho ni ishara Benchi la Ufundi la Yanga linafanya kazi nzuri kwenye uwanja wa mazoezi kulinda viwango vya wachezaji

4: PRISON walitaka mpira uchezwe juu.. Bahati mbaya kwao, viungo wao wakazidiwa Ubora na AUCHO.. Yanga wakaleta mpira chini na kuwafanya muda mwingi Prison kuutafuta mpira

5: AUCHO.. 🙌 Katikati ya Mauya na Feitoto.. Aliunga vyema timu kwa kutoa kutengeneza nafasi ya kupokea pasi na kutoa pasi sahihi katika maeneo sahihi

6: Yule DIARRA acheni kupima ubora wake kwa mikono yake. Miguu yake ni silaha hatari sana kwa wapinzani. Ni utulivu wake unaowafanya Yanga wafanye 'Build Up' kwa kutega mtego wal katika mstari wa pili wa ulinzi wa mpinzani

7: MBANGULA.. WHAT A HEADER! Mita kadhaa angani, anausubiri mpira hewani na kugonga kichwa cha nguvu.. Kile ni kitendo ambacho Mwamnyeto hategemei kukutana nacho mara kwa mara kutoka kwa mastraika wa NBC

8: Mabadiliko ya nafasi kwa Farid yameleta nguvu sana kwenye system ya Yanga.. Farid kama Inverted Winger [Mguu wa kushoto kutokea upande wa kulia] kunaifanya Back Line ya Timu pinzani ivurugike kwenye umbo lake. Lakini pia huwa inampa eneo kubwa Djuma Shabani kushambulia anapopanda!

9: Refa MwinyiMkuu ni kama alicheza mechi kwa presha kifuani mwake. Kuna matukio yalihitaji adhabu kubwa.. alipoacha, ni kama akabalansi mengine kwa kuyaacha!

10: Feitoto ...Silaha yake ya siri kama namba 10 ni uwezo wa kutafuta nafasi bila mpira mguuni. Wengi tunaona ubora wake akimalizia kazi yake lakini nafiki makocha wa Timu pinzani wanatakiwa kuanza kumlinda Fei kabla hajagusa mpira


Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments