Ticker

6/recent/ticker-posts


 

Alikamwe "Mambo 10 nilioyaona Yanga vs Dodoma Jiji..Wananchi What a Team"

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE1: HAPPY NEW YEAR WANANCHI! What A Team.. What A PERFOMANCE🙌 POINTI 3 za kibabe, MABAO 4 ya kikatili, CLEAN SHEET ya kwanza kwa Mshery.. Maisha yanataka nini tena kwa shabiki kwa Yanga?

2: DODOMA JIJI FC wamepigwa na kitu kizito sana kichwani. Walikutana na 'Menu' tofauti kabisa tofauti na waliyoitarajia.. Kosa Kubwa lilianzia kwenye 'Jeuri' ya mkoba wa mbinu za Mbwana Makata.. Kivipi?

3: Ni kujiwekea ncha ya kisu kwenye koo kuanza na viungo wawili tu dhidi ya Yanga.. Tena bila Kiungo mwenye asili ya kukaba kati yao.. Ni kama walipanga kutoa zawadi ya mwaka mpya kwa Aucho na FEITOTO

4: Hassan Nassoro na Mkandala .. Walisetiwa kwenye 'Transition' ya kutoka kujilinda kuja kushambulia.. Makata hakuwaza nini Timu ingefanya muda ambao inataka kupokonya mpira..

5: 4-3-2-1 ya Yanga ina nguvu kwenye kujenga shambulizi kutokea chini.. Quality ya Bangala na Mwamnyeto inawapa kiburi kwenye Plan hii.. Aucho kama namba 8 huwa anashuka chini zaidi kuongeza idadi ya namba ... Then Said anatoka pembeni na kuja kwenye 'Half Spaces' kuongeza idadi ya watu pia katikati.. kudili na plan hii na Quality ya Player wa Yanga unahitaji kuwa na Plan nzuri ya 'kudefend' kwenye Midblock..

6: MSHERY🙌 Sikutegemea utulivu ule katika mechi yake ya kwanza, akiwa na siku chache kwenye uwanja wa mazoezi! Well Done kijana👏

7: AUCHO.. kiungo wa viwango vya juu sana kwa ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati.. Ubongo wake huwa unatangulia sekunde kadhaa kabla ya kupokea mpira na kufanya maamuzi

8: MOLOKO.. Ni kama Tetesi za Ujio wa Denis Nkane umemshitua kutoka usingizini! What A Perfomance🙌 Kasi, akili na uamuzi wake kwenye pasi ya mwisho ilikuwa silaha ya sumu kwa mabeki wa Dodoma Jiji

9: Nkosi ana bahati sana kuzimaliza dakika zake kiwanjani bila kadi nyekundu .. Alicheza rafu nyingi sana kwa kukosa umakini. Dodoma ilihitaji msaada wake wa kuituliza safu ya kiungo ... Akaja kuvuruga zaidi

10: Well Done Mayele.. Ile Finishing ni kali sana. Bado safu ya ulinzi ya Dodoma ina makosa mengi sana.. Kama sio ubora wa kipa wao, Masalanga, kuna aibu kubwa wangeondoka nayo Taifa

Nb: kuna FANTA halafu kuna YANGA .. Utachagua unataka burudani gani 😃

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments