Ticker

6/recent/ticker-posts

Alikamwe "Mambo 10 nilioyaona Yanga vs Biashara Leo"1: MERRY CHRISTMAS & Happy New Year Wananchi🔋 YANGA wanaufunga 2021 na Kuufungua 2022 wakiwa KILELENI mwa NBC PREMIER LEAGUE✊ WHAT A WIN🙌

2: Mechi nzuri..👏 Tactically, Technically Tumeenjoy kutazama dakika 90 za mechi ya kuvutia machoni. Well Done kwa Benchi la Ufundi la Biashara! Kwanini?

3: Omary Madenge ameprove kwanini anastahili kuwa Mkurugenzi wa Ufundi. Aliwapa Yanga mtihani wa kimbinu. Kilichoiua mechi kwa upande wake ni tofauti ya 'Quality' ya wachezaji

4: Biashara walijua nguvu ya Yanga ni katikati ya kiwanja. Wakaubana uwanja kwenye kukaba na kutawanyika haraka pembeni wanapokuwa na mpira. Kuutoa mpira haraka katikati na kuuleta pembeni kuliwapa 'situation' nyingi za 1v1 .. Huko walinufaika na Ubora wa AMBROSE AWIO

5: FISTON MAYELE.. What A Goal✊ Tofauti ya Mayele na mastraika wengine.. Anaweza kukupa kitu bora hata katika siku ambazo anakuwa hayuko bora kiwanjani

6: AUCHO🙌 Tumeshaongea sana kuhusu Ubora wa mguu wake wa kushoto.. CLASS🙌 Kazi kubwa kwa sasa ni kuuongelea ubora wa ZAWADI MAUYA kama Holding Midfielder🙌

7: DJ MAUYA.. Aliuweka mchezo kwenye kichwa chake.. Akachagua kuutembeza mpira na sio kutembea na mpira. Kulia, kushoto.. macho yake yalikuwa 'busy' muda wote wa mchezo.. Nafikiri anatakiwa kuboresha Utimamu wa mwili.. Ni kama Upepo ulianza kukatika mwishoni

8: AMBROSE AWIO.. Yule winga jezi namba 9 wa Biashara anajua sana! Kasi yake, nguvu na maarifa vilifanya wengi wagundue udhaifu wa David Bryson kwenye kukaba

9: DIARRA 👏 Si bao analopenda kufungwa kiwanjani. Lakini alibaki kuwa bora kichwani. Hakupoteza umakini wake.. Save yake ya ATUPELE ndio iliwaweka YANGA mchezoni katika wakati muhimu

10: Asante Refa IKAMBI👏 Asante Djuma Shabani.. Asante Bangala.. Asante Ibrahim Ndunguli.. Mnastahili maboksi mazuri ya kufungua Usiku wa leo✊

Nb: Hata mkinuna.. Ndo imeshatokea😃

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments