Ticker

6/recent/ticker-posts


 

Anerlisa Amkashifu Ben Pol

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BUREALIYEKUWA mke wa staa wa RnB Bongo, Ben Pol ambaye ni Mkenya aitwaye Anerlisa amemkashifu jamaa huyo akimtuhumu kwa kutoheshimu ndoa yao miezi michache baada ya wawili hao kuachana.

Anerlisa ambaye wikiendi iliyopita alitua Dar kwa shughuli zake binafsi anasema aliumia baada ya Ben Pol kufunguka mambo mazito hadharani kuhusu ndoa yao.

“Kitu ambacho watu hawaelewi na kufahamu ni kwamba ndoa si kama uhusiano mwingine wowote. Ndoa ni taasisi inayopaswa kuheshimiwa na hupaswi kuizungumzia ovyo,” anasema Anerlisa anayetajwa kuwa na utajiri mkubwa.

Anasema chochote alichokuwa akikifanya Ben Pol kilikuwa kinakwenda kinyume na kile walichofundishwa baada ya wawili hao kufunga pingu za maisha.


 
“Tulikwenda kwenye kikao cha mafunzo ya kanisa ambapo tulishauriwa kutozungumza kuhusu ndoa yetu kuhusu kile kitakachotokea baada ya hapo… Mkienda tofauti na iwe hivyo, lakini kuzungumzia ilikuwa ni jambo kubwa sana,” anasema.

Anerlisa anafichua kwamba, Ben Pol alibadili dini na kuwa Muislam kabla ya kurejea Ukristo baada ya wiki mbili. Anerlisa anasema hatajutia kuchumbiana wala kuachana na Ben Pol kwa sababu anaamini kila kitu ni funzo.

Ben Pol na Anerlisa walifunga ndoa ya kifahari na kudumu takriban miaka miwili kabla ya kuachana kwa kile kilichosemekana kwamba ni usaliti. Hata hivyo, walikuwa bado hawajajaaliwa mtoto.

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments