Ticker

6/recent/ticker-posts


 

Askofu Gwajima ‘roho ya paka,’ aijibu CCM kiana

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BUREAskofu Josephat Gwajima
UNAWEZA kusema Mbunge wa Kawe (CCM), Askofu Josephat Gwajima, ana roho ngumu au ya paka, kwani licha ya chama chake, kumweka kiporo, ameendeleza kauli na misimamo kinyume na mipango ya Serikali, kuhusu chanjo ya Korona (UVIKO-19). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Askofu Gwajima, kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, amekuwa mpinzani wa chanjo hiyo, tangu Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan, iingie madarakani tarehe 19 Machi 2021 na kubadilisha mwelekeo kuhusu janga la korona, ikiwamo kutangaza idadi ya maambukizi, vifo na kuruhusu chanjo kuingia nchini.

Akizungumza wiki iliyopita, Askofu Gwajima alisisitiza, “msimamo kuhusu chanjo ya Korona bado uko pale pale.”

Aidha, jana Jumapili akiwa kanisani kwake, Ubungo, Dar es Salaam, Askofu Gwajima alijibu kiaina uamuzi wa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM, kutokana na hatua yake ya kumweka kiporo kwa kusema, “Mungu akikupa, amekupa.”

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments