Ticker

6/recent/ticker-posts

Auawa kwa Kupigwa Pembe na Ng’ombe
MWANAUME mmoja mwenye umri wa miaka 40, Joseph Weremba kutoka Kijiji cha Mtetemo, eneo Bunge la Mumias Mashariki, Kaunti ya Kakamega nchini Kenya aefariki dunia baada ya alipigwa pembela ng’ombe wake dume aliyemnunua wiki iliyopita wakati ng’ombe wake akipigana na ng’ombe mwingine wa kaka yake.

 

Taarifa iliyotolewa na baba mzazi wa wa Joseph, Jared Weremba amesema Joseph alimnunua fahali huyo wiki moja iliyopita na alikuwa akifanya mazoezi akijiandaa kwa pigano ambalo lingefanyika Disemba 26.

 

Walioshuhudia kisa hicho, walidokeza kwamba fahali wa Joseph alizidiwa nguvu kwenye pigano hilo, na kumgeukia bosi wake kisha kumpiga pembe kifuani kabla ya kumrusha upande wa nyuma. Mwendazake alivuja damu hadi kufa na mwili wake kupelekwa kwenye chumba cha kuhifadhi maiti katika Hospitali ya St Mary’s Mumias.

 

Tambiko ambalo hufanywa wakati mikasa kama hiyo ikifanyika, liliandaliwa na fahali huyo kukatwa vipande vipande. Tambiko hilo linasemakana kuwa na umuhimu wa kuwakinga wanafamilia dhidi ya mapepo ambayo yanaweza kujitokeza na kusababisha mkasa mwingine kama huo

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments