google-site-verification: googleb0bc30c3e5fdb812.html Baada ya Maneno Mengi..Yanga Waanza Mazungumzo Kumsajili CHAMA....Mwakalebela Kama Kawa | UDAKU SPECIAL

Baada ya Maneno Mengi..Yanga Waanza Mazungumzo Kumsajili CHAMA....Mwakalebela Kama Kawa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

UONGOZI wa Yanga umeanza rasmi mazungumzo na wakala wa kiungo mshambuliaji Mzambia, Clatous Chama anayekipiga Klabu ya RS Berkane ya nchini Morocco.

Hiyo ikiwa ni siku chache tangu uongozi wa Yanga kuanza mazungumzo na Berkane inayommiliki baada ya kumnunua kutoka Simba kwa dau la Sh 1Bil.

Mzambia huyo alijiunga na Berkane katika msimu huu  baada ya timu hiyo kufikia muafaka mzuri na Simba kwa ajili ya kumnunua.

Mmoja wa mabosi wa Yanga, ameliambia Championi Jumatano kuwa, wapo katika hatua za mwishoni za kukamilisha usajili wa kiungo huyo baada ya kupeleka ofa nzuri Berkane.

Bosi huyo alisema kuwa Yanga wanapata ujasiri wa kumpata kiungo huyo kutokana na ukaribu na maelewano mazuri na wakala huyo aliyefanikisha usajili wa Yannick Bangala na Shaban Djuma.

Aliongeza kuwa wakala huyo hivi karibuni alitembelea katika kambi ya Yanga huko Avic Town, Kigamboni kwa ajili ya kufuatilia mazoezi ya timu hiyo wakijiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara.

“Yanga wana asilimia kubwa ya kumsajili Chama, licha ya klabu yake ya zamani ya Simba kupewa nafasi kutokana na mkataba wake kumbana.

“Mkataba wa Chama wa kutoka Simba kwenda Berkane ni mgumu, hivyo ili asaini Yanga ni lazima wauvunje mkataba wake ambao wenyewe wapo tayari kutoa kitita chochote cha pesa ili kukamilisha dili hilo.

“Simba wenyewe wanaonekana kushindwana naye kutokana na dau kubwa la Sh 1Bil ambalo wanalihitaji Berkane ili wamuachie kiungo huyo ambaye inaelezwa hafurahii maisha ya Morocco,” alisema bosi huyo.

Alipotafutwa Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela kuzungumzia hilo alisema:

“Tupo kwenye mazungumzo na wachezaji wengi kwa ajili ya usajili wa dirisha dogo, hivyo huenda Chama akawepo au asiwepo katika mipango yetu.”

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad