Ticker

6/recent/ticker-posts


 

Chama Uso Kwa Uso na SIMBA Kombe la Shirikisho Afrika.

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

 


Simba imepangwa kundi moja dhidi ya RS Berkane ya Morocco katika Hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.


Timu hizo zipo Kundi D pamoja na Asec Mimosas ya Ivory Coast na Union Sportive Gendarmerie Nationale ya Niger, lakini gumzo kubwa nchini Tanzania ni Simba kukutana na Berkane.


Sababu kubwa ni kuwa Simba inaweza kukutana na mchezaji wake wa zamani Clatous Chama ambaye kwa sasa anaichezea timu hiyo ya Morocco lakini pia Tuisila Kisinda aliyekuwa Yanga anakutana na Simba kwa mara nyingine.


Hiyo inamaanisha kuwa Kisinda atakutana uso kwa uso na Joash Onyango huku Chama akikutana na waajiri wake wa zamani ambao pia anahusishwa kurejea klabuni hapo hivi karibuni.


Kwa upande wa makocha Florent Ibenge ambaye alishakutana na Simba mara kadhaa akiwa Vita Club, safari hii anakutana na wapinzani wake wakiwa chini ya Kocha Pablo Franco.

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments