Chillah Atingisha Kiberiti "Kuna Kitu Nikiongea Nitagawa Nchi"




MKONGWE kunako Bongo Fleva, Abubakari Shaban Katwila almaarufu Q-Chief au Chillah anafunguka kuwa, kuna kitu anacho ambacho akikiongea kinaweza kusababisha nchi kujigawa.

Akizungumza na GLOBAL PUBLISHERS, Chillah anasema kuwa, anaweza kuzungumza kila kitu, lakini watu wakahisi kama anatafuta njia ya kutokea ndiyo maana anaamua kukaa kimya ili kuruhusu maisha mengine yaendeLee.

“Kuna vitu ambavyo nilikaa kwenye kioo nikajitazama na kusema kuwa siku nikitaka kuongea kila kitu kwenye jamiii, naweza nikaigawa nchi, halafu mimi ni mtu mdogo sana, halafu kuna baadhi ya watu wanaweza wakahisi kwamba natafuta njia ya kutokea,” anasema Chillah.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad