Ticker

6/recent/ticker-posts


 

Diamond Platnumz Hana Maajabu Tena Anapoelekea ni Kama Alipokuwa Ali Kiba..Harmonize Anatisha

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE


Miaka Kadhaa iliyopita Alikiba alitawala game la Bongo Fleva lakini akaja kusimama miaka kadhaa bila kutoa ngoma, then akaibuka na "Mwana" chini ya ROCKSTAR 4000, Mwaka 2014. Baada ya kuja na ngoma hiyo akasema kwamba amekuja kufuta vumbi na kukikalia kiti chake cha ufalme wa Bongo Fleva.

Turudi nyuma kidogo, Katika kosa ambalo Alikiba alilifanya na atajutia katika maisha yake ni kukubali kusimama miaka zaidi ya miwili bila kutoa ngoma, maana wakati amesimama ndio wakati ambao Diamond platnumz alijiiamarisha zaidi na akabeba kijiji. Yani Alikiba anarudi kwenye game mwaka 2014 tayari Diamond yuko moto sana. Ngoma kama Mdogo mdogo ilikuwa on Fire.

Tangu kuzama kwa Alikiba mpaka sasa, Diamond ndio mfalme wa Bongo Fleva, ingawa Alikiba huwa anajiita Mfalme, lakini huwa anajidanganya.

Game la bongo fleva kawaida yake halina mbabe, ni kupokezana kijiti, Hivi sasa Diamond ni kama vile amezeeka kwenye game, na hana maajabu tena. Mtu hatari kwasasa ni Harmonize, na ninaamini ipo siku, wala sio muda mrefu, harmonize atamshusha tuu Diamond.


 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments