Ticker

6/recent/ticker-posts


 

Drake Achafukwa..Atangaza Kujitoa TUZO za Grammy

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE


Staa mkubwa wa Rap nchini Marekani anayekimbiza na albamu yake ya Certified Lover Boy, Drake ametangaza kujitoa katika kinyang’anyiro cha Tuzo za Grammy zinazotarajiwa kutolewa Januari 31, 2022 katika Ukumbi wa Staples Centre, Los Angeles.


Akiwa na tuzo nne za Grammy kabatini hadi sasa, Drake alitajwa kuwania tuzo katika vipengele viwili kwa mwaka 2022 ambavyo ni; Best Rap Albam kupitia albamu yake ya ‘Certified Lover Boy’ na ‘Best Rap Perfomace’ kupitia ngoma yake ya ‘Way 2 Sexy’ aliyowashirikisha Future na Young Thug.


Drake hajaeleza sababu za kujitoa katika tuzo hizo ingawa habari za chini ya kapeti zinaeleza kuwa huenda ni kwa sababu ya sakata linaloendelea la mashabiki 11 kufariki dunia na wengine wengi kujeruhiwa katika Tamasha la Astroworld la mkali Travis Scott, lililofanyika Novemba 5, 2021 ambalo Drake aliitwa kupafomu.

Cc; @bakarimahundu

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments