Ticker

6/recent/ticker-posts


 

Haji Manara awaombea wachezaji wa Simba Baada ya Kuzidiwa na Kifua na Mafua Hadi Mchezo Kuhairishwa

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BUREBaada ya kutoka kwa taarifa ya mechi ya Kagera na Simba Sc kuahirishwa kwa sababu ya wachezaji wa Simba kuumwa mafua na kifua, Msemaji wa Klabu ya Yanga Haji Manara amewaombea wachezaji wa klabu hiyo kupona haraka ili kuendelea na majukumu yao.

Kupitia Instagram yake Haji Manara ameandika kuwa

"Maradhi yanapowatokea wenzenu hata kama mna upinzani gani lazima uwaombee dua wapone haraka, ili waweze kurudi kucheza tena".

"Nimeyanukuu maneno ya King Pele alipowaombea wachezaji nyota wa Sweden walioumwa mafua,kabla ya mechi ya fainali ya kombe la dunia baina ya Waswidish na Wabrazil World Cup ya 1958 kule Stockholm"


"Na sisi wadau wa soka tunawaombea wachezaji wa Simba wapone haraka ili warejee uwanjani tena. Mimi siamini zile za ndani eti sijui mishahara sijui bonus ya kutoka sare na Yanga, naamini wenzetu wamepata maradhi na Insha'Allah watapona" ameongeza

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments