Ticker

6/recent/ticker-posts

Harmonize Afunguka Kuhusu PICHA na Ali Kiba "Mimi Ndio Niliomba Picha Hawezekani Watu Tunaotoka Nje Moja Tununiane Ugenini"


Msanii @harmonize_tz hakumbuki ni lini amewahi gombana na @officialalikiba ,hana kabisa ugomvi na huyo mtu wala hakuna sababu inayo fanya wawili hao wasiongee, Konde Boy amedai situation iliyotokea wakati wawili hao wapo Kenya kwaajili ya show zao,ilimuumiza kuona kama watu wanaotoka nchi moja wananuniana ugenini,hawa Wakenya wangewaonaje kwa mfano, hata interview aliyofanya Alikiba akiwa Kenya aliiona na alishangaa kwanini jamaa kaongea vile ila aliheshimu alicho kiongea pia.

Ilitokea Airport wote wamepanda ndege daraja moja na siti zinazofwatana,hivyo wakapiga story na baadae Harmonize akamuomba Alikiba wapige picha na wakapiga,na ni picha hiyo hiyo aliitumia kuwataka mashabiki wa Konde gang kuhudhuria show ya Alikiba jijini Mwanza, Hii ikiwa na maana ipi, kuwaonyesha watu huko mtaani kuwa hakuna shida na kama game haitakiwi kuwa na matabaka, huu muziki ni mkubwa ndani ya nchi tu lakini si nje,hasa kama kuna matabaka utapelekwaje huko nje.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments