Kim Kardashian amepiga hatua moja muhimu kuelekea kuwa Mwanasheria.
Mrembo na Mjasiriamali huyo jana ametangaza kupitia Instagram kuwa amefaulu mtihani wa wanasheria wa jimbo la California nchini Marekani ujulikanao kama baby bar.
“OMFGGGG I PASSED THE BABY BAR EXAM, Kim aliandika kwenye post hiyo ndefu akidai kuwa alifeli mtihani huo mara tatu katika miaka miwili ambayo amekuwa akisoma.
Amesema hakukata tamaa, aliendelea kusoma na kujaribu tena hadi amefaniwa kufaulu.
Ameeleza kuwa alifanya mtihani huo awamu ya tatu akiwa anaumwa Covid-19 na mwili wake ukiwa na joto kali.
Awali Kim mwenye miaka 41 ambaye hakumaliza chuo, alikuwa amepanga kuufanya mtihani huo mwaka 2022.
“Najua baba yangu angejivunia sana na hakika angeshtuka kufahamu kuwa hii ndio njia yangu sasa lakini angekuwa mshirika bora katika kujisomea,” ameandika Kim.
“Naambiwa alikuwa bingwa wa kuwatania watu ambao hawakufaulu katika jaribio lao la kwanza, lakini angekuwa mshangiliaji wangu mkubwa."
Kim alimalizia ujumbe wake kwa kutoa maneno ya faraja kwa mashabiki wake wanaopambana kufikia malengo yao.
“Weka fikira yako kwenye hilo na lifanye sababu ni hisia nzuri mno pindi unapofika kwenye upande mwingine.”