Ticker

6/recent/ticker-posts

Imefuchuka...Hivi Ndivyo Usajili wa Sure Boy Ulivyoikamua Yanga Mamilioni ya Pesa..ni Kufuru

 


USAJILI mpya wa kiungo mshambuliaji wa Yanga anayetoka Azam FC, Salum Aboubakar ‘Sure Boy’ umeigharimu Yanga jumla ya Sh Mil 80 kwa ajili ya kusaini mkataba huo wa miaka miwili.

Sure Boy alisaini mkataba huo wa kujiunga na Yanga jumanne ya wiki hii huku akiwa ameomba kuvunja mkataba wake naAzam FC hivi karibuni baada ya kuruhusiwa kurudi klabuni hapo.


Nyota huyo ni miongoni mwa wachezaji watatu waliosimamishwa naAzam FC pamoja naAggrey Morris na MudathirYahya kutokana na utovu wa nidhamu.


Chanzo kutokaYanga kimeliambia gazeti la Championi Ijumaa kuwa: “Siku ya Jumanne Sure Boy alikuwa makao makuu ya Yanga akiwa na viongozi ambapo alisaini mkataba akiwa na wakili, Simon Patrick.


“Ni mkataba wa miaka miwili huku dau alilochukua kwa ajili ya kusaini mkataba huo ni milioni 80 za Kitanzania na kwa sasa anasubiri tuAzam wamruhusu ili ajiunge rasmi naYanga.”


Alipotafutwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi yaYanga ambaye pia anahusika na usajili, DominicAlbinus, alisema: “Siwezi kuzungumzia masuala ya usajili sasa hivi mpaka mambo yote yatakapokamilika ambapo taarifa itatolewa na klabu.”

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments