Ticker

6/recent/ticker-posts


 

Kocha Chelsea Akubali Kushinda Kwa Bahati

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE


Kocha wa Chelsea Thomas Tuchel amesema kikosi cha timu yake kinabahati ya kuendelea kuongoza msimamo kwa Ligi Kuu England licha ya kutokuwa kwenye kiwango kizuri.

Tuchel ameyasema hayo baada ya The Blues kuibuka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Watford mchezo uliopigwa dimba la Watford na mabao ya Hakim Ziyech na Mason Mount yakiipa uhakika wa alama tatu na moja la Emmanuel Dennis likiwa la kufutia machozi kwa Watford.

“Hatukuwa tayari kwa ajili ya mchezo huu”, alisema Tuchel kocha wa zamani wa Paris St-Germain. “Tunatakiwa kujilaumu wenyewe. Hatukupata usawa katika matokeo, tumekuwa na bahati kushinda mechi ya leo”.

Wakati Chelsea wakipata shida ya kuvuna matokeo, Manchester City na Liverpool mwendo mdundo baada ya kushinda mechi zao na kuendelea kutoa presha kwa timu hiyo.

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments