Ticker

6/recent/ticker-posts


 

Koffi Olomidé afutiwa kosa la ubakaji lakini ahukumiwa kwa kuwazuilia wacheza densi

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BUREMahakama ya rufaa nchini Ufaransa imemuondolea mwanamuziki Koffi Olomidé kosa la unyanayasaji wa kingono, lakini ikamtia hatiani kwa kuwashikilia wanawake bila hiari yao.

Mahakama ilibatilisha uamuzi wa 2019 uliompata na hatia ya ubakaji wa mmoja wa wachezaji densi alipokuwa na umri wa miaka 15.

Lakini alipatikana na hatia ya kuwanyima wanawake uhuru wao katika jumba la kifahari huko Paris kati ya 2002 na 2006.

Atatumikia kifungo cha miezi 18 kilichoahirishwa kwa muda na kuwalipa fidia.

Mwendesha mashtaka ya umma alikuwa amependekeza ahukumiwe kifungo cha chini ya miaka minane.

Watuhumiwa wake "bila shaka hawakuridhishwa na hukumu ya unyanyasaji wa kingono kwa sababi kwa hili lilikuwa kitu cha muhimu zaidi ", alisema wakili David Desgranges ambaye alikuwa akiwawakilisha wanawake hao.

Mmoja wao alikuwa amedai kuwa aliwashambuliwa "katika mahoteli, wakati mwingine ndani ya gari... na katika studio za kurekodi muziki".

Mahakama mjini Versailles haikumpata na hatia ya unyanyasaji wa kingono, huku jaji akifutilia mbali shtaka la ubakaji kutokana na "kubadilika na wakati mwingine kukinzana" kwa ushahidi kutoka kwa waliomtuhumu.

Hata hivyo mahakama iligundua kuwa kitendo chake dhidi ya wanawake hao "kiliwanyima uhuru kwa kuwekwa chini ya uangalizi wa mara kwa mara " na washirika wake wawili ambao waliwazuilia kwenye chumba wakiwa wamefungwa nyuso zao.

Mbali na adhabu hiyo iliyosimamishwa aliamriwa kulipa faini ya euro 10,000-32,000 ($11,000-36,000) kwa kila mcheza densi.

Olomidé, ambaye jina lake halisi ni Antoine Agbepa Mumba, ni mmoja wa wanamuziki maarufu zaidi barani Afrika.

Msani huyo mwenye umri wa miaka 65 ni nyota mkubwa wa muziki wa rumba na soukous ambayo ni maarufu sana Afrika. Mojawapo ya vibao vilivyopendwa zaidi katika kazi yake ya muda mrefu ni Loi ya 1997.

Mwimbaji huyo amekabiliwa kisheria mara kadhaa hapo awali:

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments