Ticker

6/recent/ticker-posts


 

Kuna Watu Wana Hela Nyie..Mwanamuziki P Diddy ainunua kampuni yake ya zamani kwa Bilioni 17

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

 


Mwanamuziki nguli na mjasiriamali maarufu Duniani Sean John Combs mwenye kufahamika zaidi kwa jina la Kisanii P Diddy amefanikiwa kuurudisha kwa mara nyingine umiliki wa kampuni yake iliyokuwa ikitengeneza mavazi yenye brand za ‘Sean John’.


Diddy ametumia zaidi ya Dola za Kimarekani Milioni 7.5, sawa na kiasi cha pesa kisichopungua Bilioni 17 za Kitanzania ili kujimilikisha tena kampuni hiyo.


Katika mazungumzo yake kuhusu kuirudisha mikononi mwake kampuni hiyo, P Diddy ameweka wazi kuwa lengo lake la kuanzisha kampuni hiyo mnamo mwaka 1998.


Ilikuwa ni kuzalisha bidhaa za Mavazi kwa dhamira ya kuutangaza utamaduni wa muziki wa Hip Hop Duniani kote.


Ameirejesha kampuni hiyo baada ya mmiliki aliyeichukua kwake miaka kadhaa iliyopita kuyumba kiuchumi na kushindwa kuendelea kuiendesha  kampuni hiyo kongwe.

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments