Ticker

6/recent/ticker-posts


 

Lulu Diva Kwa Mara ya Kwanza Afunguka "Kikubwa Nimempumzisha Mama ya Nyumba Nawaachia"

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE


MREMBO anayekiwasha kunako Bongo Fleva na tamthiliya, Lulu
Abbas au Lulu Diva anasema kuwa, anamshukuru Mwenyezi Mungu amempumzisha salama mama yake kipenzi nyumbani kwa wazazi wa mama yake huyo, lakini mambo
mengine ya nyumba anawaachia waja.

Akizungumza na Gazeti la IJUMAA, Lulu Diva anasema kuwa, kikubwa alichofanikiwa kama mtoto wa Kiislam ni kumpumzisha mama yake sehemu salama na nyumbani kwao anakostahili na kumuombea ipasavyo, lakini mambo mengine anawaachia watu wa mitandao wanaoweza kuzungumza kila jambo bila kuchuja.

“Unajua walimwengu wana utofauti sana, ukimuona mtu anaongea, tena anaongea
kwenye wakati mgumu ambao mtu anapita wa kuondokewa na mama yake
mzazi, anazungumzia mambo ya nyumba bila hata kujua chochote, ni kuachana naye
maana kwangu kikubwa nimempumzisha mama yangu salama,” anasema Lulu Diva
ambaye alikuwa mtoto wa pekee kwa mama yake.

Hivi karibuni Lulu Diva alifiwa na mama yake na kwenda kupumzishwa kijijini kwao,
Muheza jijini Tanga ambapo huko ndiko ukaibuka mjadala kwamba, nyumba ilikuwa haifanani na ustaa wa mrembo huyo

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments