Ticker

6/recent/ticker-posts


 

Mafua Konki...Wachezaji wa Yanga Nao Waugua

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BUREKocha wa Yanga Nasreddine Nabi akiwa kwenye Mkutano na Waandishi wa Habari [Pre-Match Press Conference] amesema, kuna baadhi ya wachezaji wake ni wagonjwa kuelekea mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Tanzania Prisons.

Nabi amesema bado hawezi kuthibitisha wachezaji wangapi wanaweza kukosekana kwenye mchezo wa kesho kwa sababu itategemea na watakavyoamka kesho.

Nabi pia ametoa salamu za pole kwa klabu ya Simba kutokana na baadhi ya wachezaji wake kuumwa hivyo kushindwa kucheza mechi yao iliyopangwa kuchezwa leo dhidi ya Kagera Sugar.

Nabi amesema afya ya mchezaji ni muhimu kuliko mchezo wenyewe hivyo anawaombea wachezaji wa Simba wapone haraka ili warudi kucheza.

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments