Ticker

6/recent/ticker-posts


 

Mambo 5 Yatakayofanya Mwanamke Mpenzi Wako Akukumbuke Kila Mara Wewe Kidume

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE


Kumbukumbu njema hutia hamu ya kuwa karibu na mtu au kitu ni wazi kuwa hatupendi vitu vibaya virudi kwenye maisha yetu. Unafanyaje ili mwanamke akukumbuke ukiwa mbali naye?

1 MJALI UNAPOKUWA NAYE

Kujali sio lazima utoe hela kumpa mwanamke hapana, kuishi ndani ya hisia zake na kuguswa na changamoto zake hii humfanya kupenda kuwa karibu nawe.

2 LUGHA BORA ZAKO

Maneno ni silaha kubwa sana kwenye maisha ya binadamu. Ukiwa na maneno ya kuthamini na kumpa moyo muda wote utabaki akilini mwake.

3 UPENDO WA DHATI

Mwanamke akijua kuwa dhati ya upendo wako ipo kwake mara zote huwa anatamani kuwa na wewe. Mfanyie vitu vipya huwapo naye faragha hii itabamba hisia zake na muda wote ataijiwa na hamu yako zaidi chakula.

4 PENDA KUTOA KWAKE

Usiangalie yeye anatoa kwako au hatoi, wewe kama unacho na anakihitaji mpe. Jenga tamaduni pia ya kumpa bila yeye kukuomba. Pia jitahidi uwe unamletea zawadi hata ndogo utakaa akilini mwake.

5 HESHIMU NDUGU ZAKE

Unapoheshimu wazazi wake kama wazazi wako, na unapoheshimu ndugu zake hilo huleta faraja kubwa kwa mwanamke na muda wote hujawa na kiu yako. Heshimu watu wake atakupenda kila muda.

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments