Ticker

6/recent/ticker-posts


 

Aolewa na Ex Wake Aliyemwagia Tindi Kali...Alifungwa Jela Alivyotoka Mapenzi Yakarudi

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE


Mapya yaibuka ! Mwanadada huyo kwa jina la Berfin Ozek(20) toka nchini Uturuki amewaacha watu midomo wazi baada ya tarehe 23 December hii kukubali kuolewa na ex wake huyo ambaye alimwagia tindikali(acid) na iliyomharibu vibaya usoni na kufanya asiweze kuona tena vizuri hadi sasa 


Jamaa huyo kwa jina la Casim Ozan Celtik(23) miaka miwili iliyopita wakiwa wapenzi walipishana kauli ambapo jamaa alimwagia mrembo huyo tindikali na kumharibu uso hadi sasa, mdada alipoteza uwezo wa kuona pia. Jamaa alimwambia mdada kama huwezi kuwa na mimi basi hakuna mwanaume yeyote atakayekuwa na wewe

Mdada aliuguzwa hospitali kisha akamfungulia kesi mpenzi wake huyo na kukamatwa. Baadaye jamaa akaanza kumtumia mdada jumbe nyingi wayamalize amsamehe. Mdada amkamsamehe na kuifuta kesi. Kitu ambacho kiliwakera sana watu na kuanza kumsema mdada huyo kuwa hajielewi


Baadaye mdada akafungua tena kesi jamaa akahukumiwa miaka 13 na nusu jela. Lakini kutokana na mabadiliko ya sheria nchini humo hivi karibuni na masharti ya janga la korona jamaa ameachiliwa na kuwa chini ya uangalizi

Na baada ya kutoka jamaa hajali maneno mengi ya watu yaliyojaa ghadhabu juu ya unyama aliomfanyia mdada huyo, badala yake akamuita mdada huyo wafunge ndoa ambapo mdada amekubali wamefunga ndoa tarehe 23 mwezi huu. Licha ya kuwa kasababishiwa ulemavu wa kudumu usoni na macho hayaoni vizuri jicho moja linaona kwa asilimia 30% lakini amesema anampenda sana jamaa huyo na anadai anapendwa pia na jamaa huyo

Baba mzazi wa mdada huyo hata hivyo akihojiwa na media nchini humo ameonesha kusikitishwa sana na binti yake kutokujitambua, baba mzazi amesema wao Kama  wazazi walimpigania mtoto wao baada ya unyama aliofanyiwa lakini kilichotokea ndio hicho na hata wao kama wazazi hawakuhudhuria ndoa hiyo na wala hawakufahamu kuhusu binti yake kufunga ndoa na mtu aliyemsababishia ulemavu wa kudumu makusudi

Mmoja wa watu amesema hata kama kaamua kumsamehe lakini sheria bado ingemhukumu jamaa ili kitendo alichokifanya kisionekani ni cha kawaida wengine wapate kujifunza. Mwingine akasema kwakuwa ameamua kuwa nae karibu tena asuburi kufanyiwa janga zito zaidi ya hilo

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments