Ticker

6/recent/ticker-posts


 

Maskini Wakazi..Akatishwa Tamaa na Muziki wa Hip Hop Tanzania "Tumepoteza Mvuto Kibiashara"

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE


Rapa Wakazi amefunguka kuhusu hali ya muziki wa Hip Hop kwa sasa hapa nchini, amesema wasanii wa Hip Hop Tanzania wamepoteza mvuto wa Kibiashara hivyo ni ngumu kwa wawekezaji kuwadhamini. Wakazi amefunguka hayo wakati akijibu tweet ya mdau mmoja ambaye alitoa pendekezo kwamba, anatamani kufanyika kwa onesho moja kubwa la Hip Hop mwezi huu. Aidha @wakazi ambaye amekuwa akipaza sauti na kutoa mitazamo yake kwenye mambo mbali mbali, aliongeza kwamba hata kampuni moja ya bia ambayo imekuwa ikiupa nguvu muziki wa Hip Hop, mwaka huu wamehamia kwa Ma-DJ na sio wasanii wa Hip Hop kutokana na kukosa weledi na uwezo wa Kibiashara nyuma ya wasanii wa Singeli na Bongo fleva.

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments