Ticker

6/recent/ticker-posts

Mchungaji aliyembaka msichana mwanakwaya, Tulikuwa katika mahaba

 


Mchungaji wa kanisa la Christ Apostolic Bible katika jimbo laOgun lililopo kusini magharibi mwa Nigeria anaendelea kushikiliwa mahabusu tangu Ijumaa, baada ya kudaiwa kumbaka msichana wa miaka 16 .

Polisi katika jimbo la Ogun wanaochunguza tukio hilo wanasema mchungaji huyo alipanga na mke wake kumbaka msichana huyo ambaye ni mwanakwaya katika kanisa lao.

Lakini Mchungaji Peter Taiwo na mke wake wamekuwa wakikwepa kueleza ukweli halisi wa kilichotokea.

Mchungaji huyo anasema yeye na msichana huyo 'wamekuwa katika mapenzi na wote walipendana kimapenzi.'

"Nilimwambia aachane na mpenzi wake wa kiume na aniombe chochote anachohitaji"

Mchungaji huyo alisema wakati msichana alipoumia mguu, niliwasaidia wazazi wake kupata usaidizi wa matibabu yake.

"Kuanzia siku nilipouangalia mguu wake, msichana alianza kunitumia jumbe za mapenzi na nilikuwa nazijibu. Bado nina jumbe katika simu yangu ," alisema Mchungaji.

‘’Tuliongea nikamwambia hakuna kushiriki ngono pamoja lakini tumekuwa tukipendana’’, alisema Mchungaji na kuongeza kuwa "Wakati ule tulipoanza hatukuwa na mahusiano ya kingono, lakini tulionyeshana mapenzi," Pasta Taiwo anasema.

Hatahivyo mchungaji anakiri kuwa waliingia katika mahusiano ya ngono na msichana na kumfahamisha mke wake, ambaye hakuwa na la kusema.

Akizungumza na BBC mke wa Mchungaji alisema kuwa hakuwa anafahamu kuwa mume wake alikuwa anamtumia vibaya msichana.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments