Ticker

6/recent/ticker-posts


 

Meneja wa Harmonize Anusurika Kwenye Ajali Basi Likigonga Gari Lenye Mwili wa Marehemu

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE


MMOJA wa mameneja wanaomsimamia mwanamuziki Harmonize, Jembe ni Jembe amepata ajali mbaya ya gari wakiwa wanasindikiza mwili wa marehemu Joel Chacha aliyekuwa Injinia Mwandamizi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania iliyotokea leo Desemba 29, 2021 maeneo ya Boko jijini Dar es Salaam.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Jembe ni Jembe meneja hjuyo ameposti picha za ajali hiyo na kusindikiza na maneno yafuatayo:

Tukiwa njiani kuelekea Kumpeleka Mwili wa Mpendwa Wetu Joel Chacha,Airport;Limetokea basi liki tanua kwa kasi na kugonga msafara wetu ikiwa pamoja na kuharibu vibaya gari iliyo kuwa imebeba Mwili wa Mpendwa wetu, hapo Boko tegeta.

Wote tumetoka salama kasoro wachache majeruhi akiwapo dereva wa Gari la Mwili,wamewahishwa hospitali.Nimetaarifiwa Dereva anaendelea Vema. Thanks GodπŸ™πŸΌ

Bus hilo Lilikua Linaelekea Tanga Wanasema linaitwa HD,😑 Limeendelea kwa kasi na kutoweka huku kukiwa na Abiria.Tunaomba Askari mlioko njia ya Tanga mumsimamishe dereva huyu Inaonekana hayupo sawa..Na achukuliwe hatua kali.Aidha Apimwe akili nk.

UNAWEZAJE KUGONGA GARI NNE IKIWEMO MWILI WA MAREHEMU NA USISIMAME WALA KUSTUKA??Dah! Tunamshukuru Mungu kwa kila Jambo πŸ™πŸΌ na Tuombe Safari ya Joel iwe salama mpaka kaburini Kwake TarimeπŸ™πŸΌπŸ˜­ Leo toka asubuhi Nimesimama na Neno la Mungu Kutoka Zaburi 91:14-16.

Asante sana @theprayermirror Kwa Neno hili La Uzima.Thanks Pamela @pamelabhoke for your Text,few Minutes before the accident.πŸ™πŸΌ♥️

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments